Tunafanya nini

Tunatekeleza miradi katika uwanja wa maji na miundombinu ya usafi ambapo pia tunaunda ajira. Tunatekeleza miradi yetu katika eneo la mastangoni karibuna mji wa kilifi katika nchi ya Kenya. Tunafanya kazi sasa kwa miradi hii:

  • Ujenzi wa visima katika matsangoni
  • Kujenga vyoo na bafu (flush, shower and go) katika vijiji vitano (5) vya matsangoni

Ujenzi wa visima

Wenyeji wa Matsangoni huchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa visima vya maji wenyewe. Shirika letu linawasaidia wakati wa ujenzi. Matsangoni ni kijiji cha wakaazi elfu sita (6,000). Kwa sasa hakuna vifaa vya usafi au visima vya maji. Philip Kadenge Kahindi, mwenyekiti wa tawi letu la Kenya na mwanzilishi wa mradi huu, alihifadhi fedha kwa mdawa miaka sita (6) ili kuwezeshwa kuwekesha kisima na tanki la maji katika nyumba yake mwenyewe. Sasa yeye anataka wakaazi wengine wa matsangoni wawe na urahisi wa kupata hali ya usafi. Kwa hivyo ameweza kuwasiliana na shirika letu miongoni mwa mambo mengine, juu ya msingi wa wazo la shirika na kuchangia mradi wenyewekila familia inalipa euro mia tano (500) (kama euro 4.25) kila mwezi na kwa kufanya hivyo, anahifadhi fedha kwa ajili ya saruji, mchanga, matofali na ajira.

Ujenzi wa visima
Ujenzi wa visima

Choo na bafu (flush, shower and go)

Tulikamilisha mradi wa majaribio wa choo na bafu (flush, shower and go) katika mwaka wa 2014. Tulifanya hivyo kwa kushirikiana na GetItDone (kupata kufanyika) na pia kwa harambee. Jingo kwa ajili ya choo na bafu (flush,shower and go) ni kituo cha umma cha usafi ambapo wanakijiji wanaweza kuoga, kwenda choo na kunawa mikono yao. Picha zifuatazo hapa chini zitakupa hisia ya kuundwa kwa mradi huu wa majaribio.